BUDAPEST: Maadhimisho ya mapinduzi ya mwaka 1956 nchini Hungary, yachafuliwa na maandamano ya upinzani
24 Oktoba 2006Matangazo
Maandamano dhidi ya serikali ya Hungary yameathiri maadhimisho ya mwaka wa 50 tangu kuanguka kwa utawala wa kikoministi mwaka wa 1956. Polisi wamelazimika kutumia gesi za kutoa machozi na risase za mpira kuwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Budapest. Kwa uchache watu 128 wamejeruhiwa na wengine kiasi ya 100 wamekamatwa na kuzuwilia na polisi.
Purkushani imeendelea hadi leo asubuhi. Wajumbe kutoka nchi 50 wamehudhuria sherehe za maadhimisho hayo ya mapinduzi ya mwaka 1956. Sherehe zimefanyika mbele ya jengo la bunge. Ujerumani imewakilishwa na rais Horst Köhler.