BUDAPEST: Hungary yaomboleza wahanga wa uasi wa 1956
5 Novemba 2006Matangazo
Kiasi ya watu 50,000 wameandamana nchini Hungary kuadhimisha uvamizi wa Soviet Union ya zamani kuzima uasi dhidi ya ukomunisti katika mwaka 1956.Miaka 50 iliyopita,Hungary ilivamiwa na vikosi vya Kisoviet kukandamiza mapinduzi maarufu na takriban raia 3,000 wa Hungary waliuawa. Maandamano ya Jumamosi yaliyoitishwa na chama kikuu cha upinzani cha mrengo wa kulia Fidesz, yalifanywa pia kulalamika dhidi ya matumizi ya nguvu ya polisi.Kama majuma mawili ya nyuma,katika maandamano ya kuipinga serikali,zaidi ya watu 100 walijeruhiwa kwa risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi