1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSLES: Umoja wa Ulaya umetoa azimio juu ya mpango wa nyuklia wa Iran

11 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CElt

Umoja wa Ulaya umetoa azimio kwa shirika la nishati ya nyuklia la umoja wa mataifa, linalolenga kuishawishi Iran kusitisha shughuli zake zote za nyuklia. Msemaji wa shirika hilo amesema azimio hilo litajadiliwa wakati wa mkutano wake mjini Vienna, nchini Austria baadaye hii leo.

Haya yanafanyika baada ya Iran kuondoa mihuri ya umoja wa mataifa katika kinu chake cha nyuklia cha Isfahan, hivyo kukiruhusu kuanza kazi kamili. Hatua hii itaiwezesha Iran kusafisha madini ya uranium ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia.

Ujerumani na Marekani ni baadhi ya mataifa yaliyoikosoa Iran kwa kuchukua hatua hiyo. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani amewaambia waandishi habari mjini Washington kwamba Marekani itajitenga mbali na serikali ya Tehran.