1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels.Umoja wa Ulaya watenga Euro milioni 16 kwa ajili ya uchaguzi Kongo.

4 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFP

Umoja wa Ulaya umetenga kiasi cha Euro milioni 16 kusaidia uendeshaji wa uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuziba pengo lililokuwepo.

Kiasi hicho kinafanya msaada uliotolewa na nchi hizo kufikia Euro milioni mia moja na sitini na tano.

Wakati huo huo Kamishna wa maendeleo wa Umoja wa Ulaya Luis Michel amewataka wagombea wakuu rais Joseph Kabila na mpinzani wake Jean-Pierre Bemba waheshimu matokeo ya uchaguzi wa awamu ya pili utakaofanyika tarehe 29 mwezi ujao.