1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:.Uingereza ingali kushikilia msimamo wake juu ya nafuu inayopokea kutoka bajeti ya Umoja wa Ulaya

16 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF3D

Uingereza bado inakaidi kwamba haiwezi kukubaliana juu ya mzozo wa nafuu ya euro bilioni 5 inayopewa katika mchango wake wa bajeti.

Waziri mkuu wa Luxembourg Jean Clode Junker,ambaye ataongoza mkutano huo wa kilele wa viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya wa siku mbili amesema huenda akashindwa kulitatua suala la bajeti ya Umoja wa Ulaya.

Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na tofauti miongoni mwa viongozi hao.

Rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso amesema Umoja huo huenda ukakumbwa na mzozo wa muda mrefu hadi pale viongozi wa Umoja huo watakapofikia makubaliano juu ya bajeti ya Umoja huo ya Mwaka 2007 hadi mwaka 2013 na katiba ya Umoja huo.

Barosso ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari,siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa kilele wa Umoja wa ulaya mjini Brussels.