BRUSSELS.Mvutano waendelea juu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya
17 Juni 2005Matangazo
Wanadiplomasia wanasema mkutano wa viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels haujafikia maendeleo yoyote juu ya suala la mzozo wa nafuu ya mabilioni ya Euro inazopokea Uingereza kutokana na mchango wake kwenye bajeti ya Umoja huo.
Hata hivyo Uingereza imesema italijadili suala hilo iwapo tu kiwango kikubwa cha ruzuku ya wakulima wa Ulaya kitapunguzwa hatua ambayo inapingwa vikali na Ufaransa ambayo inafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na sera hiyo.
Mjadala huo wa bajeti umekuja baada ya viongozi hao kukubaliana hapo jana kuongeza muda wa kuidhinisha katiba mpya ya Umoja huo baada ya katiba hiyo kukataliwa na wafaransa na waholanzi.