1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Kusitishwa kwa kanuni za bajeti Ulaya sio halali

7 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFlG
Mawaziri wa Fedha wa Umoja wa Ulaya wamechukuwa hatua kinyume na sheria wakati walipositisha kanuni za bajeti za Umoja wa Ulaya ili kuiepushia Ujerumani na Ufaransa hatua za adhabu kutokana na kuwa nakisi iliopindukia mno.
Hayo ni maoni ya kisheria yaliowasilishwa leo hii kwa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya.Duru za Umoja wa Ulaya zinasema Kamishna wa Uchumi na Masuala ya Fedha Pedro Solbes atapendekeza kwamba chombo hicho kikuu cha Umoja wa Ulaya kipinge uamuzi huo wa mwezi wa Novemba katika Mahkama ya Haki ya Ulaya kwa kuzingatia maoni hayo ya kisheria.
Hatua hiyo itazidi kuchochea malumbano kati ya Kamisheni hiyo ikiwa katika siku zake za mwisho madarakani na nchi wanachama zikiongozwa na mataifa makubwa ya kiuchumi barani Ulaya Ujerumani na Ufaransa.