BRUSSELS:Kampuni ya Microsoft yatozwa faini ya Euro 280 na tume ya Ulaya
12 Julai 2006Tume ya Ulaya imeitoza faini ya zaidi ya Euro millioni 280 kampuni ya Microsoft kwa kushindwa kuzingatia sheria za kupinga ushindani.
Kampuni hiyo kubwa ya Software imekabiliwa na sakata hiyo kufuatia mzozo wa muda mrefu kati ya shirika moja la Marekani na wanaopanga kanuni za kibiashara wa Umoja wa Ulaya.
Uamuzi uliotolewa umefuatia hukumu ya kihistoria iliyotolewa na Umoja wa Ulaya mwaka 2004 ambapo Microsoft iliagizwa kutoa maelezo kwa makampuni mengine juu ya mfumo wa uendeshaji shughuli zake.
Kampuni ya Microsoft imesisitiza kwamba inayafuata maagizo ya tume hiyo na imesema faini iliyotozwa sio ya haki.
Kampuni ya Microsoft imefahamisha kwamba ilitarajia kutoa maelezo mengine zaidi ya mwisho juu ya maelezo ya uendeshaji wa shughuli zake yanayotumiwa na makampuni mengine ya Computa ifikapo tarehe 18 mwezi huu.