1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Algeria kusaidiwa na NATO kupambana na ugaidi

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAY

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za magharibi NATO Bwana Jaap de Hoop Scheffer anaahidi kuisadia nchi ya Algeria kupambana na ugaidi kufuatia mlipuko wa mabomu hapo jana mjini Algiers.

Jumuiya hiyo inaimarisha ushirikiano wake na mataifa kadhaa ya kusini mwa Meditarranean ikiwemo Algeria.Kupambana na ugaidi ulimwenguni ni moja ya mambo muhimu katika ajenda ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO inayoshirikisha mataifa 26.