1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUbelgiji

Brussels yaimarisha usalama kuelekea mkutano wa kilele wa EU

27 Juni 2024

Usalama umeimarishwa mjini Brussels wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya wakikusanyika kwa ajili ya mkutano wa kilele wa siku mbili.

https://p.dw.com/p/4hZaU
Wakuu wa Umoja wa Ulaya wamewasili Brussels kwa ajili ya mkutano wa kilele wa siku mbili.
Wakuu wa Umoja wa Ulaya wamewasili Brussels kwa ajili ya mkutano wa kilele wa siku mbili.Picha: Nick Gammon/John Thys/AFP/Getty Images

Viongozi hao wanatarajiwa kujadiliana juu ya nafasi za juu za uongozi kwenye umoja huo pamoja na hali katika eneo la Mashariki ya Kati na Ukraine.

Ajenda nyingine kwenye mkutano huo ni usalama na ulinzi na ushindani ndani ya Umoja wa Ulaya.

Viongozi wa mataifa hayo ya Ulaya bado hawajafikia makubaliano ya mwisho ya mgombea wa nafasi hizo, lakini baadhi wamenukuliwa wakiisifu rekodi ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Ursula von der Leyen, anayeonekana kurejea kwenye nafasi hiyo kwa awamu ya pili baadaye mwezi huu.