1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wasi wasi kuhusu uchaguzi wa Ethiopia

17 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMD

Umoja wa Ulaya umeeleza wasi wasi wake kuhusika na ripoti za unyanyasaji,vitisho na watu kutiwa jela nchini Ethiopia kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa nchini humo mwezi ujao.Umoja wa Ulaya vile vile umekosoa uamuzi wa serikali ya Ethiopia kuanzisha sheria itakayowapiga marufuku wasimamizi wa kienyeji walio elfu kadhaa.Kwa wakati huo huo Brussels haikuridhika na uamuzi uliopitishwa mwezi wa Machi na serikali ya Addis Ababa kuyafukuza makundi matatu ya kidemokrasia ya Marekani.Umoja wa Ulaya unapeleka Ethiopia zaidi ya wajumbe 150 kusimamia uchaguzi wa tarehe 5 mwezi Mei.Huo utakuwa uchaguzi wa kwanza kufanywa chini ya usimamizi wa kimataifa nchini Ethiopia.