1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Umoja wa Ulaya wataka kusitishwa kwa uhasama Lebanon.

2 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDPc

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya wametoa taarifa ya pamoja inayotoa wito wa kusitishwa kwa uhasama katika mashariki ya kati.

Lakini hawakutoa wito rasmi wa kusitishwa mapigano.

Nchi kadha , ikiwa ni pamoja na Ujerumani na Uingereza zimezuwia wito wa kusitishwa mapigano ambao ulikuwamo katika muswada wa mwanzo wa taarifa hiyo.

Mkuu wa masuala ya sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Javier Solana amesema kuwa jumuiya ya kimataifa inahitaji kuunda mara moja jeshi la kulinda amani katika Lebanon.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Finland Erkki Tuomioja , ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kilichochukua saa kadha mjini Brussels amewaambia waandishi wa habari kuwa maana ya wito huo inabaki kuwa hivyo licha ya mabadiliko katika uandishi wake.

Pia amekanusha kuwa kumekuwa na mgawanyiko mkubwa ndani ya kundi hilo la mataifa 25 wanachama wa umoja wa Ulaya juu ya kuushughulikia mzozo wa sasa wa mashariki ya kati.