BRUSSELS : Umoja wa Ulaya umeliweka suala la umaskini juu katika agenda ya Umoja wa Mataifa
13 Septemba 2005Umoja wa Ulaya umetowa wito kwa viongozi wa dunia kufanya jitihada zaidi kufikia muafaka juu ya mageuzi yaliopendekezwa kwa Umoja wa Mataifa wakati watakapokutana hapo kesho katika Mkutano wao wa Kilele mjini New York.
Wajumbe wamekuwa katika majadiliano kuelekea kwenye mkutano huo lakini bado ingali wanatafautiana juu ya masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na usalama,haki za binaadamu na maendeleo.Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso amesema kwamba mataifa tajiri yanapaswa kuyakinisha upya ahadi ya kutowa misaada zaidi ya maendeleo.Lakini Marekani inakataa kujifunga na ahadi yoyote ile.Umoja wa Ulaya umetangaza vita dhidi ya umaskini katika nchi zinazoendelea kuwa ni mada muhimu kabisa ya Mkutano huo wa Kilele wa Umoja wa Mataifa.
Takriban watu milioni 800 wanateseka na utapia mlo duniani kote.