BRUSSELS: Slovenia kutumia Euro kuanzia mwaka 2007
11 Julai 2006Matangazo
Sarafu ya Euro itaanza kutumiwa nchini Slovenia mwaka 2007.Uamuzi huo umepitishwa na mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya mjini Brussels.Slovenia itakuwa mwanachama wa 13 katika kile kinachojulikana kama “kanda ya Euro.”Slovenia ambayo hapo zamani ilikuwa nchi ya kikomunisti,sasa katika muda usiotimia hata miezi sita inapaswa kuchapisha noti za Euro na kutengeneza centi za Euro.Nchi zingine zinazongojea kujiunga na kanda ya Euro ni Estonia,Cyprus na Malta.