1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Sheria za bajeti zikikiukwa zitaathiri Euro ,ECB.

22 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFUm

Benki kuu ya umoja wa Ulaya imeonya kuwa mabadiliko ya kupunguza makali ya sheria za bajeti za umoja huo yanaweza kuiathiri sarafu ya Euro. Mawaziri wa fedha wa umoja huo wamekubaliana siku ya Jumapili kupunguza makali ya maafikiano ya umoja huo juu ya uthabiti na ukuaji, ambapo serikali zinaruhusiwa kuongeza deni lake, na kupindukia kiwango kilichowekwa cha pengo la bajeti kwa baadhi ya masharti. Baraza la utawala la benki hiyo limesema kuwa linawasi wasi mkubwa na mabadiliko hayo yaliyopendekezwa, likisema kuwa yanaweza kuleta matatizo katika mfumo wa kiuchumi wa jumuiya ya Ulaya.

Hata hivyo kansela Gerhard Schroeder ameyafurahia mabadiliko hayo ambayo yanaipa Ujerumani nafasi ya pekee kutokana na gharama zake kubwa za muungano.

Ujerumani na Ufaransa zimekuwa zikikiuka kiwango kilichowekwa cha kutovuka asilimia 3 ya pengo la bajeti kwa muda wa miaka mitatu sasa.