1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. NATO kutoa usafiri kwa wanajeshi wa mataifa ya Kiafrika watakao linda amani huko Dafur.

10 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF59

Mawaziri wa ulinzi wa mataifa wanachama wa NATO wanaokutana mjini Brussels wameidhinisha mpango wa kuwapeleka wanajeshi wengine 5 000 zaidi wa mataifa ya Afrika katika jimbo lililokumbwa na machafuko nchini Sudan la Dafur.

Huu utakuwa ujumbe wa kwanza wa umoja huo katika bara hilo.

Idhinisho hilo la NATO kwa ajili ya operesheni hiyo inakuja siku moja kabla ya mazungumzo kuhusu amani ya Dafur yanayosimamiwa na umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Umoja wa mataifa unakadiria kuwa kiasi cha watu 180 000 wameuwawa katika jimbo hilo na zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuyahama makaazi yao tangu mapigano yaanze hapo Februari 2003.

Shirika la NATO linapanga kuwa tayari na ndege za kusafirishia kuazia Julai mosi.