BRUSSELS: NATO kuimarisha vikosi Afghanistan
26 Januari 2007Matangazo
Mawaziri wa nje wa nchi zilizo katika shirika la kujihami NATO,wanakutana hii leo mjini Brussels kushauriana juu ya kuimarishwa vikosi vya shirika hilo nchini Afghanistan.Kamanda wa NATO,Jemadari David Richards amearifu kuwa vikosi zaidi vitapelekwa Afghanistan ambako shirika hilo tayari lina wanajeshi 33,000.Marekani katika mkutano wa Brussels inataka kuwashinikiza wanachama wenzake kutoa mchango zaidi katika eneo la Hindukutch.Baada ya mkutano huo,serikali ya Ujerumani itaamua ikiwa ipeleke Afghanistan,ndege za upelelezi za aina ya Tornado.