BRUSSELS: Mwito kusitisha mapigano kati ya Hamas na Fatah
15 Mei 2007Matangazo
Umoja wa Ulaya umetoa mwito wa kusitisha moja kwa moja mapambano mapya yaliozuka kati ya makundi hasimu ya Hamas na Fatah.Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,machafuko hayo mapya yanahatarisha juhudi za kupata suluhisho la amani kwa mgogoro wa Mashariki ya Kati.Mwito huo umetolewa baada ya kuripotiwa kuwa wanachama wanane wa tawi la walinzi wa Rais Mahmoud Abbas wameuawa na wanamgambo wa Hamas. Kwa upande mwingine,Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu,Amr Moussa ameutuhumu Umoja wa Ulaya kuhusika na msimamo wake wa kukataa kujadiliana na Hamas.Chama cha Kipalestina cha Hamas kimetajwa katika orodha ya makundi ya kigaidi ya Umoja wa Ulaya.