1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS Mawaziri wa NATO kukutana mjini Brussels hapo kesho

8 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF5e

Mawaziri kutoka mataifa wanachama wa jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi ya NATO watakutana hapo kesho mjini Brussels kujadili njia za kuwasaidia walinda usalama wa umoja wa Afrika walio katika eneo la Darfur nchini Sudan. Shughuli za ugavi bado zinaandaliwa pamoja na umoja wa Ulaya.

Shirika la NATO na umoja wa Ulaya zimeahidi kuusaidia umoja wa Afrika, unaopanga kuiongeza mara mbili idadi ya wanajeshi wake wa kulinda amani katika eneo la Darfur mwezi ujao. Umoja wa Afrika umeahidi kuisadia serikali ya Sudan kuwapokonya silaha wanamgambo wa janjaweed na kurudisha usalama katika eneo la Darfur.