Brussels. Jumuiya ya Ulaya yaitaka Ethiopia kuacha vitisho dhidi ya wapinzani kabla ya uchaguzi mkuu hapo May.
17 Aprili 2005Matangazo
Jumuiya ya Ulaya imeeleza wasi wasi wake juu ya ripoti kuwa kunatokea bughdha, usumbufu, kukamatwa watu na vitisho nchini Ethiopia kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Jumuiya ya Ulaya pia imeulaumu uamuzi wa serikali ya Ethiopia wa kuanzisha sheria ambayo inapiga marufuku mamia ya waangalizi wa uchaguzi kutoka nchini humo, kushiriki katika kazi hiyo. Jumuiya ya Ulaya haifurahii uamuzi wa Ethiopia uliofikiwa mwezi March kuyafukuza makundi matatu ya kidemokrasia ya Marekani.Jumuiya ya Ulaya inatuma zaidi ya wachunguzi 150 katika uchaguzi wa May 5 nchini Ethiopia ambao utakuwa wa