1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Jumuiya ya Ulaya kutoza kodi tiketi za ndege ili kugharamia misaada ya maendeleo katika nchi masikini.

14 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDb

Mawaziri wa fedha wa jumuiya ya Ulaya wamekubaliana kuweka kodi maalum kwa tiketi za safari za ndege ili kusaidia kugharamia misaada ya maendeleo ya ziada kwa ajili ya mataifa masikini.

Waziri mkuu wa Luxembourg Jean – Claude Juncker amesema kuwa mpango huo utakuwa kwa ujumla ni wa kujitolea kwa mataifa wanachama , mashirika ya ndege na wasafiri. Hakuna tarakimu ama kiwango kwa ajili ya kodi hiyo kilichojadiliwa.

Austria hata hivyo imepinga mpango huo kuwa ni mzigo kwa watumiaji wa huduma hiyo na ni uharibifu wa hali ya ushindani baina ya mashirika ya ndege na kusema kuwa haitashiriki katika mpango huo.