BRUSSELS: Japan yaahidi itasaidia NATO katika harakati zake nchini Afghanistan.
13 Januari 2007Matangazo
Japan imeahidi kuwa na mwelekeo mpya katika ushirikiano wake wa kijeshi na jumuiya ya NATO.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe aliyetembelea makao makuu ya NATO mjini Brussels, amesema Japan itasaidia harakati za NATO kukabiliana na wanamgambo nchini Afghanistan kwa kutoa misaada ya kiutu na misaada mingine isiyo ya kijeshi.
Katiba ya Japan inaikataza nchi hiyo kuwa na majeshi ya kutumiwa vitani ila tu kwa jukumu la kujilinda kutokana na uvamizi wa mataifa ya nje.
Waziri Mkuu Shinzo Abe kwa sasa hivi yumo nchini Ufaransa kwenye awamu ya mwisho ya ziara yake katika mataifa manne ya Ulaya.