1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS :Ghana yashikilia Mugabe kualikwa kikao cha EU-AU

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1g

Nchi ya Ghana iliyo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU inashikilia kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aalikwe katika mkutano wa Umoja wa Ulaya na Afrika unaopangwa kufanyika mwezi Disemba.Kulingana na Waziri wa mambo ya kigeni wa Ghana Nana Kufo Addo Umoja huo haupaswi kuchagua raia wa Kiafrika atakayehudhuria mkutano huo unaoshirikisha bara zima.

Mkutano huo wa pili umeahirishwa mara mbili na unapangwa kufanyika mjini Lisbon nchini Ureno mwezi Disemba.Kuwako kwa Rais Mugabe katika mkutano huo kunatisha kuvunjika tena kwani Umoja wa Ulaya una tashwishi na mkwamo wa kisiasa nchini Zimbabwe.

Rais Mugabe na wasaidizi wake wamepigwa marufuku kufanya safari za Ulaya baada ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2002 kwa kukiuka haki za binadamu.Mkutano huo ulipangwa kufanyika mwezi Aprili mwaka 2003.