BRUSSELS: Gates ayatembelea makao makuu ya NATO
15 Januari 2007Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates yumo mjini Brussels Ubelgiji katika ziara yake ya kwanza kwenye makao makuu ya shirika la NATO. Ziara yake hiyo inalenga kujadili idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan, mzozo wa Darfur nchini Sudan na wasiwasi wa kuzuka machafuko katika jimbo la Kosovo.
Waziri Gates ametokea mjini London ambako alisema Uingereza ni mshirika wake mkubwa muhimu kwa Marekani nchini Afghanistan na Irak.
Gates aliyasema hayo kufuatia mkutano wake na waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair na waziri wa ulinzi Des Browne mjini London.
Gates alizuru London kuujadili mpango mpya wa rais George Bush kuhusu Irak na mpango wa Uingereza wa kutaka kuyaondoa majeshi yake kutoka kusini mwa Irak.