BRUSSELS: Ethiopia yatuhumiwa kukiuka sheria za kidiplomasia
21 Oktoba 2006Matangazo
Umoja wa Ulaya umeituhumu Ethiopia iliyowafukuza wanadiplomasia wawili wa Umoja wa Ulaya na kusema hicho ni kitendo kisichoweza kukubalika na kimekiuka sheria za kidiplomasia.Afisa wa Umoja wa Ulaya kutoka Sweden,Bjoern Jonsson na mwenzake,Enrico Sborgi kutoka Italia walipewa muda wa saa 24 kuondoka Ethiopia,kufuatia madai kuwa walijaribu kuwapeleka Kenya watoro wawili. Watu hao wawili ni Waethiopia waliokuwa wakifanya kazi na Halmashauri ya Ulaya.Ethiopia imesema, watu hao wamekamatwa kuhusika na uhalifu mkubwa lakini haikutoa maelezo zaidi.