1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRAZZAVILLE:Kongo na Brazil zaafikiana kushirikiana katika miradi ya maendeleo

17 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7F6

Jamhuri ya Kongo na Brazil zimetiliana saini mikataba ya afya na kilimo katika ziara ya siku moja ya Rais wa Brazil Luiz Ignacio Lula Da Silva.

Rais Wa Jamhuri ya Kongo Deniss Sassou Nguesso anapokea vizuri wito wa Rais da Silva wa mageuzi ya nishati mbadala baraani Afrika yaliyozinduliwa rasmi nchini Burkina Faso.Rais Nguesso anaelezea nishati hiyo kama chanzo cha maendeleo katika bara la Afrika lililo na rasilmali nyingi.

Nchi hizo mbili zimeafikiana kushirikiana katika miradi ya kupambana na kuzuia malaria na HIV nchini Kongo aidha kutoa mafunzo ya wafanyikazi pamoja na ushirikiano wa teknolojia ya uzalishaji.

Kiongozi huyo wa Brazil anasema huenda taifa lake likasaidia Kongo kulipa deni lake la kigeni na anaunga mkono majadiliano kati ya Kongo na Shirika la Fedha Duniani IMF.

Rais Da silva anahudhuria mkutano wa IBSA unaofanyika nchini Afrika Kusini.