Brazil yatia fora Afrika
14 Novemba 2007Ingawa zimetenganishwa na bahari ya Atlantik,Brazil na Angola, zimeungana kwavile sio tu zazungumza lugha moja-kireno bali pia kwa historia zao ndefu kama koloni la mreno.Isitoshe, biashara kati ya Angola na Brazil wakati huu, inazidi kustawi kuliko wakati wowote kabla.
Brazil,dola kuu kabisa huko Amerika Kusini, ambalo wakaazi wake milioni 1888 na ukubwa wake wa kilomita za mraba milioni 8.5 ni zaidi ya nusu ya eneo na wakaazi wa bara zima la Amerika kusini,yabainika imevinjari kuchukua usukani kutoka mikono ya Ureno kama mtiaji mkubwa zaidi wa raslimali kwa nchi za kiafrika zinazozungumza kireno.
Katika kipindi chake kinachokaribia miaka 5 madarakani,rais Luiz Inacio Lula da silva wa Brazil amezuru bara la Afrika mara saba.
Afrika kusini na Nigeria pia ni washirika muhimu kibiashara na Brazil barani Afrika,lakini koloni za zamani za mreno ndio shabaha hasa :Hizo zajumuisha nchi kama Angola,Visiwa vya Cape Verde,Guinea-Bissau,Msumbiji na sao Thome na Principe.Kundi la nchi hizi limegeuka shina la diplomasia ya kisiasa na kiuchumi ya Brazil.
Angola ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba milioni 1.25 na wakaazi wanaopindukia milioni 15,ni mzalishaji wapili mkubwa kabisa wa mafuta barani Afrika baada ya Nigeria.
Uhusiano wa biashara katiu ya Angola na Brazil ulianza kukua hapo 2000 wakati wa serikali ya rais Cardoso,lakini tangu rais Lula kushika madaraka Januari 2003,raslimali za Brazil zimeongezeka mno nchini Angola.
Jumuiya ya ya makampuni ya Brazil nchini Angola (AEBRAN) kwa ufupi,inasema kuwa biashara kati ya nchi hizi mbili imeongezeka mara 6 tangu 2002 na ingali ikikua.
Katika warsha iliofanyika Luanda hapo Septemba,mwaka huu kuadhimisha mwaka wa 185 tangu kujikomboa Brazil kutoka utawala wa Ureno, waziri wa fedha wa Angola Jose Pedro de Morais alisema kuwa kiwango cha fedha kinachomiminwa Angola na Brazil kilifikia dala milioni 475 kwa mwaka 2006.
Bidhaa inazosafirisha Brazil nchini Angola, ziliongezeka kwa kima cha dala milioni 520 mnamo mwaka 2005 na kufikia dala milioni 836 mwaka jana 2006.Na mnamo miezi 9 ya kwanza ya mwaka huu ,bidhaa hizo zilipanda kwa kima cha 14% kutoka kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Braztil inaiuizia Angola hasa mashini,zana za matumizi ya majumbani,vipuri vya magari,matrekta,zana za mawasiliano ya simu na za uchimbaji mafuta ya petroli.Inaiuzia Angola hata mafuta kutokana na kasoro iliopo Angola ya vinu vya kusafishia mafuta.
Brazil nayo huagiza kutoka Angola,mafuta ya petroli yasiosafishwa kwa kima cha dala milioni 460 hii ikiwa mwaka 2006.
Idadi ya makampuni ya Brazil nchini Angola imeongezeka kwa kima cha 70% mnamo miaka 5 iliopita.
Wabrazil kwahivyo, wameanza kumiminika katika nchi ambayo mbali na mafungamano ya kihistoria na ya kilugha, takriban haikujulikana sana hadi mwongo mmoja tu uliopta.Wabrazil 5.000 waishio nchini Angola wanafanya kazi hasa katika viwanda vya ujenzi,madini na vya kilimo.Zaidi katika majimbo ya Cabinda, Lunbda Norte na Malanje lakini pia katika mji mkuu Luanda.
Kwa miaka mingi, pamekuwapo mabingwa wachache tu waliotumika katika koloni za zamani za mreno barani Afrika kutoka Brazil.Badala ya kuwaweka kando wakoloni wa zamani-wareno,wabrazil wanaimarisha idadi yao na hii inakaribishwa mikono miwili na makamo waziri wa nje wa Ureno, Joao Gomes Carvinho.