1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brazil yaomboleza baada ya mkasa wa ndege

Thelma Mwadzaya19 Julai 2007

Viongozi kote ulimwenguni wanatoa rambi rambi zao kwa jamaa za waliopoteza maisha yao kwenye ajali mbaya ya ndege kuwahi kutokea nchini Brazil..Ndege aina Airbus 320 ilidondoka mjini Sao Paulo hapo jana na kusababisha vifo vya abiria wote 200 waliokuwa safarini

https://p.dw.com/p/CB2i
Mabaki ya ndege ya A320 iliyodondoka
Mabaki ya ndege ya A320 iliyodondokaPicha: AP

Ndege hiyo ilidondoka kwenye uwanja wa ndege wa Congonhas na kushika moto baada ya kugonga bohari moja. Ujerumani vilevile Ufaransa zinajitolea kuwapa wataalam 4 wa uchunguzi katika mkasa huo wa ndege.Chama cha Usafiri wa ndege nchini Canada cha Montreal nacho kinajitolea kusaidia katika uchunguzi wa mkasa huo.Wataalam wengine 5 wa kampuni ya ndege ya Airbus wako njiani kuelekea kwenye eneo la mkasa.

Ndege hiyo iliteleza kwenye barabara ya ndege inayoelezwa kuwa fupi mno kwa ndege ya aina hiyo katika uwanja wa ndege wa Congonhas ulio mjini.

Kwa mujibu wa kiongozi wa Shirika la Ndege la TAM Marco Antonio Bologna hakuna manusura wowote.Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anatangaza siku 3 za maombolezo ya kitaifa.

Wakati huohuo chama cha wanasheria nchini Brazil Orden de los Abogados, OAB kinatoa wito kwa wahusika wote wa ajali hiyo kujiuzulu.