Brazil yajiandaa
Brazil inajiandaa kwa jukumu kubwa. Kujiandaa kwa Dimba la Kombe la Dunia na Michezo ya Olimpiki katika miaka miwili. Wabrazil wanaisubiri michezo hiyo kwa hamu hata kama mambo hayaendi kwa kasi.
Nchi yajawa na msisimko
Siku zinaendelea kuhesabiwa tayari kwa kombe la dunia. Wakati timu ya taifa ya Brazil ikiendelea kujiimarisha, mashabiki tayari wamejawa na msisimko. Mashabiki wa kabumbu wa Brazil wanaonekana kuwa machachari sana kote ulimwenguni, na hata katika picha hii, filimbi zao ni kama zina kelele nyingi kuliko vigelegele vyao.
Ataipa Brazil kombe la dunia?
Ni maarufu sana miongoni mwa Wabrazil. Neymar, mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22, ambaye sasa anaichezea FC Barcelona. Ni chipukizi anayetambulika na takribani wafuasi milioni 7 kwenye ukurasa wa Twitter. Wengi wana matarajio makubwa kuliko uzani wake wa kilo 65.
Mradi wa bilioni moja
Serikali ya Brazil inataka kutekeleza mpango mkubwa wa miundo mbinu. Inajenga viwanja vya ndege 800, barabara za umbali wa Kilometa 7,500 na barabara za reli za umbali wa Kimoleta 10,000. Kiasi cha jumla cha uwekezaji: Euro bilioni 52 katika miaka ijayo. Kufikia sasa, miundo mbinu iliyopo haiwezi kwenda sambamba na ukuwaji uchumi wa Brazil.
Wageni milioni 28
Hata kama ni mahali pa kuwavutia wageni wengi kwa ajili ya likizo, Brazil sasa ni makao mapya ya tamasha za fainali ya Kombe la Dunia 2014 na Michezo ya Olimpiki 2016. Watalaamu wanataraji kutakuwa na watu milioni 28 watakaoitembelea Brazil. Lakini sasa uwezo wa hoteli katika vitovu vya kitalii kama Copacabana ni haba na vya bei ghali.
Gharama kubwa za ujenzi
Sifa mbaya iliyoenezwa iliathiri ujenzi wa viwanja vya michezo. Ukarabati wa uwanja wa Maracanã mjini Rio sasa unagharimu Euro milioni 500. Uwanja wa Itaquerão mjini São Paulo uliokabiliwa na mgogoro wa kisheria usilisimamishwa na haijulikani ni vipi utatumiwa katika siku za usoni.
Afadhali uwe salama kuliko kujuta
Zaidi ya euro milioni 700 zimewekezwa katika upanuzi wa mfumo wa usalama wa serikali ya Brazil kwa matamasha kubwa kama vile Kombe la Dunia na Olimpiki. Hii ni pamoja na kuwekwa vituo 12 vya usalama katika miji itakayokuwa mwenyeji pamoja na ununuzi wa ndege zisizoruka na rubani ili kufanya doria za angani.
Treni maalum katika mitaa ya mabanda
Hapa pia, mashabiki wa kombe la dunia wanastahili kusafiri kwa kasi: Complexo do Alemão mjini Rio, ni mojawapo ya "favela" kubwa zaidi (mitaa mikubwa sana ya mabanda) nchini Brazil. Tangu mwaka wa 2011 treni maalum zakuning'inia zinazohudumu kutoka kwenye maeneo ya mabanda – usafiri usio na malipo kwa wakaazi, ambao pia huwavutia watalii.
Kombe la dunia ni fursa
Siyo tu kwamba kombe la dunia ni fursa kubwa kwa Brazil, lakini pia kwake Fabiano Fernandes. Hadi hivi karibuni, akiwa gerezani, amekuwa akishiriki katika ujenzi wa uwanja mpya wa Brasilia. Anajivunia, kusaidia kuujenga na kisha kuwa na matumaini ya kuwa baadaye anaweza kuwachiliwa huru.
Nyota wa kesho
Wakati Wabrazil wote sasa wakisubiri kwa hamu na ghamu, kazi katika Copacabana tayari inaendelea. Watoto wa shule ya kandanda ya “Energia” wanajifunza teknolojia ya kabumbu, katika sehemu ambayo huwa ngumu: mchangani. Mlinda lango Cleidijames anaota kuwa simu moja atakuwa mchezaji mwenye ujuzi.
Furaha mikononi mwake
Ni mashabiki wangapi kama Jarbas Carlini wanaotarajia kuliona taji la sita la ulimwengu kwa Brazil? Tayari ana ishara ya bahati nzuri mikononi mwa Brazil: kombe la zamani na la sasa la ulimwengu – hata kama ni la bandia.