1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRASILIA: Brazil na Marekani zakubaliana kushirikiana kibiashara

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKs

Rais wa Brazil na rais wa Marekani wamekubaliana kushirikiana katika mkataba wa biashara ya kimataifa na kuitanzua mizozo iliyopo katika mahusiano yao ya kibiashara. Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amesema mataifa yote mawili yanatambua umuhimu wa kumalizika kwa ufanisi mkubwa mazungumzo ya Doha ya shirika la biashara duniani, WTO.

Rais George W Bush amesema ipo haja ya kuanzisha eneo la soko huru la kibiashara litakalozijumulisha Amerika kazkazini na kusini. Rais Bush sasa yumo Panama kwa mazungumzo zaidi.

Ziara yake katika mataifa ya Amerika ya kati na kusini imegubikwa na maandamano yaliyojaa machafuko yaliyofanywa na watu wanaoipinga sera ya Marekani na mkataba wa kibiashara.