Botswana yafanya uchaguzi mkuu
30 Oktoba 2024Zaidi ya watu milioni moja wamesajiliwa kupiga kura katika taifa hilo la kusini mwa Afrika lenye utajiri wa almasi. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa asubuhi hii huku wagombea wanne wa urais wakiwa katika kinyang'anyiro cha kuliongoza taifa hilo lililopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1966 wakati chama cha Botswana Democratic - BDP kilichukua madaraka.
Soma pia: Botswana yenye utajiri wa mafuta kufanya uchaguzi wa bunge, Jumatano
Wapiga kura katika nchi hiyo wameelezea wasiwasi kuhusu kudorora kwa uchumi na ukosefu wa ajira ambao umefikia asilimia 27 ya kura, huku kukiwa na madai ya rushwa serikalini na usimamizi mbaya wa madaraka.
Muungano mkuu wa upinzani ni Umbrella for Democratic Change - UDC, ukiongozwa na mwanasheria wa haki za binaadamu, Duma Boko mwenye umri wa miaka 54.