Ajali ya boti yaua takribani watu 50 Kongo Mashariki
3 Oktoba 2024Idadi kamili ya waliokuwamo kwenye boti hiyo haikufahamika mara moja na kwamba ni watu watu wangapi waliokuwemo ndani ya boti hiyo na ni wangapi ambao wameangamia.
Mashuhuda wamesema watoa huduma ya uokozi walisaidia kutoa miili 50 kwenye maji huku watu 10 wakinusurika na kupelekwa katika hospitali ya mtaa.
Maafisa wa Kongo mara nyingi wameonya dhidi ya upakiaji kupita kiasi na kuapa kuwaadhibu wanaokiuka hatua za usalama kwa usafiri wa majini.
Soma pia:Raia wakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula Goma
Lakini katika maeneo ya mbali ambako abiria wengi wanatoka, wengi hawawezi kumudu usafiri wa umma kutokana na uchache wa barabara.
Itakumbukwa pia mnamo mwezi Juni, Boti iliyokuwa imejaa mizigo ilizama karibu na mji mkuu wa Kinshasa na abiria 80 walipoteza maisha.