Boti 9 za wahamiaji zakamatwa zikijaribu kuingia Uingereza
10 Novemba 2024Jaribio hilo la kuvuka kuingia nchini humo limefanyika wakati Waziri Mkuu Keir Stammer akiwa kwenye juhudi mpya za kuyawinda magenge ya walanguzi yanayowasafirisha watu kupitia mataifa ya magharibi ya Balkani ili kuwazuia wahamiaji kufika nchini humo. Idadi hiyo inaifanya idadi jumla ya wahamiaji waliowasili Uingereza kufikia 32,691 kwa mwaka huu.
Soma zaidiWatu 30 wakamatwa kwa magendo ya binaadamu Uingereza:
Siku ya Alhamisi, Stammer alitangaza makubaliano ya kuhamasisha kushirikishana taarifa za kiitelijensia, utaalamu na mataifa ya Serbia. Macedonia Kaskazini na Kosovo.
Waziri Mkuu huyo wa Uingereza ameapa pia kuwashughulikia walanguzi hao kama magaidi huku akiongeza bajeti ya pauni milioni 75 kwa askari wa mipakani. Kwa mwaka huu pekee, hadi sasa wahamiaji karibu 50 wameshakufa maji wakati wakijaribu kuvuka ujia wa bahari kuingia Uingereza, kulingana na walinzi wa Pwani ya Ufaransa.