Borussia Dortmund yaibwaga Celtic 7-1
2 Oktoba 2024Matangazo
Timu nyingine ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, ilipata ushindi wa tabu wa bao 1-0 dhidi ya Milan nyumbani BayArena.
VfB Stuttgart walilazimishwa sare 1-1 nyumbani na Sparta Prag.
Soma zaidi: Dortmund yaanza kampeni ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Club Brugge
Katika matokeo mengine, Arsenal ilionesha ubabe Paris Saint Germain kwa kuicharaza mabao 2-0, huku Manchester City ikiitandika Slovan Bratislava goli 4-0.
Leo Bayern Munich inakwaana na Aston Villa huku RB Leipzig ikiwa na miadi na Juventus.