1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund yadhibiti kipindi cha kwanza cha ligi

Sekione Kitojo
24 Desemba 2018

Borussia Dortmund imetamalaki katika nusu ya kwanza ya msimu huu wa Bundesliga lakini mabingwa Bayern Munich wamezinduka  kuoka katika hali ya kwikwi hali ambayo inaleta matumaini ya mpambano mkali mwishoni.

https://p.dw.com/p/3Ab0i
Fußball: Bundesliga | Bayer Leverkusen - Borussia Dortmund
Picha: picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd

Borussia  Dortmund  huenda  ina  historia  upande  wake  wakati wakiwa  na uongozi wa  pointi  sita  katika  kipindi  hiki  cha mapumziko  ya  majira  ya  baridi  lakini  itakuwa  ujinga  kuwapuuzia Bayern Munich  kwa  kuwa  ligi  hii  ya  Ujerumani  hatimaye  itakuwa na  mpambano  mkali  wa  kuwania  ubingwa kwa  mara  nyingine tena.

Deutschland Borussia Dortmund v Borussia Moenchengladbach - Bundesliga | Götze und Reus
Marco Reus(kulia) na Mario Goetze(kushoto)Picha: Getty Images/Bongarts/L. Baron

Dortmund  imeweza  kunyakua  taji  la  ubingwa  wakati  wakiongoza katika  kipindi  hiki  cha  mapumziko  ya  katikati  ya  msimu , na vijana  chipukizi  wa  kocha  Lucien Favre  wameng'ara   katika michezo  17  iliyopita.

Ushindi  mara  13, sare  mbili  na  kipigo  mara  moja  tu na  tarakimu zilizo  wazi  wakati  wakijikingia  pointi 42, jumla  ya  pili  bora  katika historia  ya  klabu  hiyo  licha  ya  kuwa  kocha  mpya  Lucien Favre ameomba  kuwe  na  subri  na  kikosi  chake  kipya  kuelekea mwishoni  mwa  msimu.

Fußball Bundesliga Eintracht Frankfurt - Bayern München Ribery torjubel
Frank Ribbery akishangiria bao dhidi ya Eintracht FrankfurtPicha: picture-alliance/dpa/U.Anspach

Usajili wa katikati ya mwaka

Lakini wachezaji  walionunuliwa  katikati  ya  msimu  ambao  ni pamoja  na  mlinzi Abdou Dialo  pamoja  na  wachezaji  wa  kati Thomas Delaney  na  Axel Witsel  hadi  mshambuliaji  Jadon sancho na  Paco Alcacer  wamekosha  nyoyo  wapenzi  wa  Dortmund pamoja  na  nahodha wao  ambaye  yuko  katika  kiwango  cha  juu Marco Reus  wakati  Dortmund  ina  matumani  kwa  mara  ya kwanza  kunyakua  taji  la  ubingwa  tangu  mwaka  2012.

"Tunamatumaini  tutaendelea  kuwa  fit  na  kuendelea  kufanya vizuri. Kutokana  na  hali  hiyo  mengi  yatawezekana,"  amesema Reus.

Deutschland Bundesliga - Eintracht Frankfurt v Bayern München | Tor Rafinha
Wachezaji wa Bayern wakifurahia bao dhidi ya Eintracht FrankfurtPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Dortmund inapata kujiamini  sana  katika  kipindi  hiki  cha mapumziko  wakati  wakiumaliza  mwaka  kwa kurejea  katika mafanikio  baada  ya  kupata  kipigo  cha  kwanza  katikati  ya  wiki, dhidi  ya  timu  iliyoko  mkiani  ya  Fortuna Dusseldorf  kwa kuishinda  Borussia  Moenchengladbach kwa  mabao  2-1 katika  kile kilichoelezwa  kuwa  ni  pambano  la  timu  zilizoko  juu  ya  msimamo wa  ligi siku  ya  Ijuma.

Mkurugenzi  wa  soka   wa  Gladbach Max Eberl ameitaja  Dortmund kuwa wana  uwezekano  mkubwa  wa  kupata  taji la  ubingwa  lakini ameonya  kwamba "hakuna  mtu  anapaswa  kuipuuzia  Bayern.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae