BONN.Mabadiliko ya hali ya hewa yajadiliwa Bonn
7 Mei 2007Matangazo
Wajumbe wa serikali na wataalamu kutoka nchi zaidi ya 100 duniani wamekutana hapa mjini Bonn Ujerumani kwenye kikao kilichoandaliwa na Umoja wa mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Mkutano huo wa wiki mbili utajadili masuala muhimu ya kutafuta njia mbadala kwa rasimu ya Kyoto katika kupunguza utoaji wa gesi chafu inayosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Rasimu ya Kyoto inamalizika muda wake mwaka 2012.Nchi zinazochafua zaidi mazingira Marekani,China na India bado hazijatia saini mkataba wa Kyoto na mojawapo ya malengo ya mkuztano huu wa Bonn ni kutafuta njia ya kuzisshawishi zisaini mkataba mpya.