1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bonn. Ujerumani yaanzisha majadiliano ya kuisaidia Afrika.

6 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEL8

Mkutano wenye lengo la kuboresha mpango wa upelekaji wa misaada ya maendeleo katika bara la uko katika siku yake ya pili leo hapa mjini Bonn. Hii ni sehemu ya juhudi za rais Horst Köhler wa Ujerumani zinazojulikana kama ushirikiano na Afrika.

Juhudi hizo zina lengo la kufungua majadiliano kati ya mataifa yenye utajiri wa viwanda na Afrika.

Mkutano huo unawaweka pamoja wanasiasa, wasomi na viongozi wa shughuli za biashara kujadili mikakati mipya maendeleo kwa bara la Afrika.

Jana Jumamosi kulifanyika maandamano makubwa ya Waethiopia wapatao 400 nje ya ukumbi wa mkutano huo wakipinga dhidi ya serikali ya waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi, ambaye yuko mjini Bonn kwa akihudhuria mkutano huo.

Siku nne za ghasia nchini Ethiopia zimesababisha watu zaidi ya 40 kupoteza maisha . Upande wa upinzani unasema kuwa serikali imefanya udanganyifu katika uchaguzi mkuu bunge , May mwaka huu.