1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN: Kimbunga kikali chavuma barani Ulaya

19 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZh
Idadi ya wanasayansi wa Kiafrika walioko Ujerumani ni ndogo
Idadi ya wanasayansi wa Kiafrika walioko Ujerumani ni ndogo

Kimbunga kikali kabisa kupata kuvuma barani Ulaya tangu miongo kadhaa,kimeua watu wasiopungua 27,miongoni mwao,7 ni nchini Ujerumani.Kimbunga hicho kilichokuwa na mwendo wa hadi kilomita 200 kwa saa kimengoa miti,mapaa na kimepindua malori kwenye barabara kuu.Nchini Ujerumani,huduma za misafara ya mbali ya treni zimesitishwa na kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt zaidi ya safari 100 zimefutwa.Nchini Uingereza nako nyumba elfu kadhaa zimekosa umeme.