1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BONN: Deutsche Welle yailaumu Serikali ya Uzbekistan

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF7

Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle Erik Betterman, amelaumu kile alichokiita uingiliaji mkubwa unaofanywa na serikali ya Uzbekistan kwa waandishi habari wa Deutsche Welle idhaa ya Kirusi.

Wiki iliyopita huko Tashkent Uzbekistan waendesha mashtaka walianza uchunguzi dhidi ya mwandishi wa kujitegemea anayefanyia kazi DW huko Uzbek, Natalya Buschuyeva.

Wakili wa mwandishi huyo amesema kuwa anatuhumiwa kwa kufanyakazi bila ya kuwa na kibali cha serikali ya Uzbekistan.

Uzbekistan imekuwa ikichukua hatua kali dhidi ya vyombo vya habari vya nje, toka vyombo hivyo viliporipoti juu ya askari wa nchi hiyo kufyatua risasi katika kundi la waandamanaji huko Andizhan mwaka jana.