1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Bonde la Afghanistan linalojivunia vijana wanaojitoa muhanga

9 Juni 2023

Wananchi katika bonde la Tangi lililoko mkoa wa vilimani mashariki mwa Afghanistan wanajivunia namna vijana wadogo wanavyojitoa muhanga ili kuwa mashahidi wa kidini, katika kile kinachotajwa kuwa vita vya Jihad.

https://p.dw.com/p/4SNGV
Afghanistan Taliban
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Eneo la Bonde la Tangi lenye wakaazi takribani 22,000 kwa kiasi kikubwa lilikuwa chini ya udhibiti wa kundi la Taliban wakati wa vita vya miongo miwili wakati Marekani na washirika wake wa Jumuiya ya NATO walipokuwa wakipambana na wanamgambo hao haswa baada ya kuondoa utawala wa kwanza wa Taliban mwaka 2001.

Vikosi vya Marekani vilishikilia upande uliokuwa ukipakana na bonde hilo na mara kwa mara vilifanya msako wa usiku vikiwatafuta wanachama wa Taliban.

Ismail Ashaqullah ni kijana aliyepatiwa mafunzo na Taliban ya kujitoa muhanga yani kujilipua na hivi leo anajuta kwanini hakutekeleza jambo hilo wakati wa vita vya Afghanistan kama walivyo mamia ya vijana kutoka eneo lake.

Soma pia:Wanajeshi wa kigeni wako katika tahadhari baada ya shambulio la IS Afganistan 

Ismail amepigana kwa miaka minane akiwa na Taliban dhidi ya vikosi vya kigeni vikiongozwa na Marekani na vikosi vya serikali ya Afghanistan.

Lakini kujiondoa kwa vikosi vya kigeni mwaka 2021 nchini humo, na kuanguka kwa serikali iliyokuwa ikiungwa mkono nchi za magharibi, ilimaanisha kwamba Ismail hakuweza kupata nafasi ya kutekeleza dhamira yake.

"Nilikuwa nikifanya Jihad lakini haikunitosheleza. Kwahiyo nilifikiria kufanya oparesheni itakayosuuza mioyo ya Waislamu kote ulimwenguni na wangu pia".

Afghanistan | Trainierter Selbstmordattentäter | Ismail Ashuqullah
Katika picha hii iliyopigwa Mei 25, 2023, mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliefunzwa na Taliban Ismail Ashugullah akitokwa machozi wakati wa mahojiano na AFP katika kijiji cha Otarhi kilichoko bonde la Tangi, wilaya ya Saydabad, mkoa wa Maidan Wardak. Ashuqullah anajuta kukosa fursa ya kujiripua wakati wa kilele cha vita vya Afghanistan, kama walivyofanya wengi kutoka bonde la Tangi.Picha: Wakil Kohsar/AFP

Tukirejea katika bonde la Tangi, ni kwamba uvamizi uliokuwa ukifanywa na vikosi vya Marekani katika eneo hili ulitajwa kukiuka desturi za kimila kwa kuvamia nyumba ambako wanawake walikuwa wakiishi kwa mfumo wa kujitenga wanaume na na wanawake na hilo liliwakasirisha Waafghanistan wengi.

Soma pia: NATO, jeshi la Afghanistan wauwa raia wengi zaidi ya Taliban

Abdul Wahab Siraj kijana mwingine anayejitolea katika kujilupua anasimulia kwamba "hatukuwa na silaha za kushindana nao kwahiyo tukaona ni vyema tukajizatiti na milipuko na kuingia sehemu za kuwahifadhi makafiri ili kuwavunja taya na kuifanya mifupa yao kuwa majivu”.

Mashambulizi ya kujitoa muhanga yalikuwa ni alama ya Taliban na sio tu katika kusababisha vifo vya watu wengi lakini pia kuongeza hofu iliyoenea.

Taliban wanadai kuwa wapiganaji wa kigeni na wanajeshi wa Afghanistan walikuwa ndio wanalengwa kila mara, lakini raia nao walijikuta kuwa sehemu kubwa ya wahanga wakiwemo wanawake na watoto.

Mashambulizi ya kujitoa muhanga kama njia ya kufanikisha azma

Kwa mujibu wa ripoti ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, mwaka 2019 pekee kulikuwa na watu 1,499 waliouawa kutokana na mashambulizi ya kujitoa muhanga yaliyofanywa na Taliban.

Mashambulizi yalianzia kwa washambuliaji waliovalia fulana za kujitoa mhanga wakilenga misafara ya vikosi vya kigeni hadi matukio ya kulipua miundombinu ya kijeshi inayohusisha magari yenye vilipuzi na watu wenye silaha wanaojifanya polisi.

Afghanistan Frauenbildung
Familia ya msichana mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa muhanga wa mripuaji wa kujitoa muhanga ikiomboleza mjini Kabul, Afghanistan, Septemba 30, 2022.Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Soma pia: UN: Watoto wengi wameuwawa Afghanistan 2016

Michael Semple, Profesa katika Taasisi ya Amani na Usalama katika Chuo Kikuu cha Queens nchini Ireland anasema washambuliaji hao kwa kawaida walikuwa vijana na waliaminishwa kuwa walikuwa bora kuliko jamii nyingine.

Anaendelea kusimulia kwamba wakati wa mafunzo "wanahimizwa kuamini kwamba ulimwengu huu tunamoishi leo sio muhimu sana" na kwamba "utukufu uko katika kifo cha ushahidi."

Katika Bonde la Tangi, Mir Aslam Amiri mwenye umri wa miaka 60 ambaye alipigana dhidi ya uvamizi wa kisovieti katika miaka ya 80, anazungumza kwa fahari kubwa juu ya "mafanikio" ya mtoto wake Najeebullah mwenye umri wa miaka 20 kama mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Alipohitimu kutoka madrassa, nilimwambia, 'Mwanangu! Nenda kaanze jihadi... Makafiri wameikalia kwa mabavu nchi yetu kwa hivyo unapaswa kufanya jihadi sasa'.

Anadai kuwa hajawahi kumuona mwanawe akiwa na furaha kama siku aliyoondoka kukamilisha dhamira yake mwaka 2014.

Baadae alipoelezwa juu ya kifo chake alimwambia mkewe Amina: "Hongera sana, mwanao amekufa shahidi."

Chanzo: afpe