Bomu laua wapita njia wanne Lebanon
16 Januari 2008BEIRUT:
Watu wasiopungua watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la bomu lililotokea katika mtaa mmoja unaopatikana katika Beirut kaskazini. Miongoni mwa waliofariki katika shambulio hilo ni wapita njia wanne.Inaonekana shabaha ya shambulio hilo huenda ilikuwa gari la ubalozi wa Marekani. Na mjini Washington msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani-Sean McCormack amehakikisha gari la Ubalozi liliharibiwa na dereva wake alijeruhiwa kidogo, na kuongeza kuwa hakuna raia wa Marekani yeyote alieuawa.
Lebanon imekumbwa na milipuko kadhaa ya mabomu, na mingi imelengwa kwa wanasiasa na waandishi habari ambao wanapinga Syria.
Shambulio la sasa limekuja kabla ya kikao cha bunge,kinachonuiwa kumchagua rais baada ya hatua hiyo kuahirishwa mara kadhaa.Uchaguzi umepangwa kufanyika januari 21.Urusi imelaani shambulio hilo.