Bomu lalipuka ndani ya basi Nairobi
15 Desemba 2013Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulizi hayo---la hivi punde likiwa ni mripuko uliotokea ndani ya basi moja la abiria mjini Nairobi Jumamosi jioni, ambao uliwauwa watu watano---na hakuna aliyekamatwa kufikia sasa. Kenya imekuwa ikilengwa na mfululizo wa mashambulizi tangu ilipoyatuma majeshi yake katika nchi jirani kupigana na wanamgambo wa al-Shabaab wenye mafungamano na alQaeda, mnamo Oktoba 2011. Mashariki ya Kenya, katika mpaka wa Kenya na Somalia, ndilo eneo linalolengwa zaidi.
Watalaamu wanasita kuweka mahusiano yoyote kati ya mgogoro wa kivita na alShabaab na mashambulizi hayo ya karibuni. Mwangalizi mmoja wan chi za magharibi ameliambia shirika la AFP kuwa kufikia sasa, “hakuna ushahidi” wa kuyahusisha mashambulizi hayo na harakati za kundi hilo la Somalia.
Ijumaa iliyopita mtu mmoja aliuawa na wengine watatu wakajeruhiwa katika milipuko miwili iliyotokea kwenye soko moja la mji wa Wajir, kilomita 100 kutoka mpaka wa Somalia. Siku ya Jumanne, watu wanane wakauawa, ikiwa ni pamoja na polisi watano, katika eneo la Garissa karibu kilomita 20 kutoka mpaka wa Somalia baada ya gari walimokuwa wakisafirisa kushambuliwa katika tukio la uvamizi.
Polisi mwengine hajulikani aliko kufuatia shambulizi hilo. Na shambulizi la jana Jumamosi la basi lililiripua basi hilo, na kuliacha kuwa mabaki ya mabati na vyuma kutapakaa kila mahali. Watu watano waliawa wengine zaidi ya 40 wakajeruhiwa.
Pia kulikuwa na shambulizi lisilo la kawaida dhidi ya watalii katika mji wa Mombasa, ambao una wakaazi wengi wa kiislamu. Gruneti lililorushwa kwa gari lililokuwa likiwasafirisha watalii wa Uingereza liligonga dirisha, lakini halikuripuka. Mnamo mwezi Septemba 2011, mtalii wa Uingereza David Tebbutt aliuawa wakati akipigana na watekaji nyara katika eneo moja la kitalii mjini Mombasa, siyo mbali sana na Somalia. Mkewe, Judith, alitekwa nyara na kupelekwa Somalia, ambako aliachiwa baada ya miezi sita ya kushikiliwa maiteka.
Katika mwaka huo, mwanamke mmoja wa Kifaransa aliyekuwa akiishi nchini Kenya, Marie Dedieu, alitekwa nyara na watu waliokuwa na bunduki kutoka Somalia, kutoka nyumbani kwako Lamu, kusini mashariki mwa Kenya, na akafa baadaye. Mnamo mwezi Septemba mwaka huu, wanamgambo walilivamia jumba la maduka la Westgate mjini Nairobi na kuwauwa watu 72. lakini maafisa kazika maeneo ya mipakani na mengine nchini humo wanajua kuwa mara nyingine huwa kuna mizozo mikubwa baina ya makabila inayosababishwa na masuala kama vile maji au malisho ya mifugo, ambayo huchochewa na wanasiasa wa kutoka maeneo hayo.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo