Serikali ya Kenya imezidi kukosolewa juu ya hatua ya kuondolewa kwa zaidi ya wakaazi 3,000 katika kijiji cha Kibos kilichopo Kisumu na makazi yakiharibiwa. Hatua hii imewaacha maelfu ya waathiriwa wakitegemea misaada na kutafuta hifadhi kwenye mahema yaliyojengwa katika ardhi ya muda wakisubiri kujua hatma yao. Mwandishi wetu kutoka magharibi mwa Kenya Musa Naviye alituandalia ripoti hii.