Bolsonaro alishiriki njama ya mapinduzi dhidi ya Lula
27 Novemba 2024Matangazo
Polisi ya Brazil imedai katika ripoti yake iliyotolewa kwa umma jana Jumanne kwamba rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro alishiriki kikamilifu katika njama ya mapinduzi kumzuia mrithi wake Luiz Inacio Lula da Silva asiingie madarakani.
Ripoti hiyo ambayo imewasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa Brazil Paulo Gonet pia imesema Bolsonaro alifahamu fika mpango unaodaiwa kuandaliwa na wanajeshi wa kikosi maalumu kumuua Lula, makamu wake na jaji wa mahakama ya juu kabisa ya Brazil.
Mwanasheria mkuu anayachunguzha madai hayo mazito kuona kama ushahidi unaunga mkono madai yanayowasilishwa dhidi ya Bolsonaro na watu wengine 36 washirika katika njama hiyo.