Boko Haram yauwa watu 38 Nigeria
18 Februari 2015Kundi la Boko Haram limeapa kuuvuruga kuchaguzi huo. kwa uchaguzi huo ambao awali ulipangwa Februari 14 na maafisa wa serikali wameonesha matumaini kwamba operesheni za kijeshi katika kanda hiyo zinaweza kudhibiti vitendo vya umwagikaji damu kabla ya tarehe mpya ya uchaguzi.
Lakini mfululizo huu wa mashambulizi ya sasa ambayo yanalalamikiwa kufanywa na waasi, yanadhihirishwa changamoto kubwa kwa Nigeria na mataifa jirani, ambayo ni Cameroon, Chad na Niger, pamoja na kuwepo kwa taarifa za mafanikio za operesheni yao ya pamoja iliyoanzishwa mapema mwezi huu.
Vitisho vya kiongozi wa Boko Haram
Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau alisema"Uchaguzi huu hauwezi kufanyika hata tukiwa tumekufa" Kiongozi huyo aliyasema hayo katika mkanda wa video uliosambazwa na kundi hilo katika mtandao wa Twiter. Aidha kiongozi huyo aliendelea kusema "Mnadai hatuwezi kupambana, lakini tumelazimisha majeshi yenu kukimbia katika kambi zao na tumefanikisha kuachiwa huru kwa ndugu zetu wafungwa mlikuwa mkiwanyanyasa katika makambi yenu. Wakushuriwa pekee ni Mungu"
Akizungumza kabla ya kitisho cha Shekau, Rais wa Niger Mahamadou Issoufou alisema taifa lake litatangaza tamati ya kundi hilo ambalo katika kipindi cha miaka sita limeweza kuuwa kiasi ya watu 13,000. Akizungumza mbele ya umma wa waandamanaji, wenye kupinga Boko Haram mjini Niamey alijigamba kuwa Niger ndio itakayohakikisha kifo cha Boko Haram.
Lakini kwa hakika kundi hilo limeendelea kuonekana madhubuti na kuzusha maswali kwa wachambuzi wengi kama inawezekana likashindwa katika vita hivyo katika kipindi kifupi.
Katika jimbo la Borno, nchini Nigeria wauwaji watatu wa kujitoa mhanga walifyatua mabomu yao katika eneo la ukaguzi kwenye kijiji cha Yarmakumi, karibu na mji wa Biu na kusababisha vifo vya watu 38 na wengine 20 kujeruhiwa.
Chanzo kutoka hospitalini kililiambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba wengi wa waathirika walikuwa watoto wenye kufanya shughuli za uchuuzi na ombaomba ambao kwa kawaida wanakusanyika kwa wingi katika eneo la kituo hicho cha ukaguzi.
Boko Haram limekuwa likirejea mara kadhaa kuteka mji wa Biu, ulipo kiasi cha kilometa 180, kutoka mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri, lakini limekuwa likifurushwa na majeshi ya Nigeria na wanamgambo wenye dhamana ya usalama katika eneo hilo.
Muda mwingine wa masaa kadhaa baadae katika mji wa Potiskum, mji wa kibiashara wa jimbo jirani la Yobe,huko huko kaskazini mwa Nigeria mtu mwingine aliyejitoa mhanga alijirupua katika mgahawa mmoja maarufu katika eneo hilo. Meneja wa mgahawa aliuwawa na wahudumu 13 walijeruhiwa vibaya.
Katika hatua nyingine jeshi la Chad limesema vikosi vyake vimekabiliana na mapigano makali na Boko Haram karibu na mji wa Dikwa, kiasi ya kilometa 90 kutoka Maiduguri.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman