1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA,Rais wa zamani wa Colombia afariki

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjh

Rais wa zamani wa Colombia Alfonso Lopez Michelsen amefariki.

Alfonso aliyefariki hapo jana akiwa na umri wa miaka 94 alipigia debe mpango ambao hatimaye uliifanya Marekani kurudisha mfereji wa Panama kwa Panama mwaka 1977.

Rais wa Panama Martin Torrijos amezungumzia masikitiko yake juu ya kifo hicho cha Lopez akisema alikuwa rafiki na mshirika mkubwa wa Panama katika mapambano yake ya kutafuta uhuru wake.

Katika taarifa nyingine mjane wa aliyekuwa rais wa Marekani Lyndon B Jonson ,Claudia Alta Taylor Jonson amefariki akiwa na umri wa miaka 94.

Bibi Claudia aliyejulikana kama Lady Bird Jonson alifariki nyumbani kwake Texas hapo jana baada kuugua kwa muda mfupi.