1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA:32 wafa katika ajali ya mgodi nchini Colombia

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUw

Wachimba mgodi wasiopungua 32 wamekufa kutokana na miripuko ya gesi aina ya methane ndani ya mgodi wa makaa ya mawe nchini Colombia.

Ajali hiyo imetokea katika jimbo la NORTE de SANTANDER kaskazini-mashariki mwa Colombia.

Habari zinasema hadi sasa ni maiti nne tu zilizopatikana.

Juhudi za kuwafikia wahanga wengine zinashindikana kutokana na msongamano wa gesi za sumu ndani ya mgodi.