1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA: Rais wa Ujerumani azuru Colombia

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJU

Rais wa Ujerumani Horst Köhler yamo nchini Colombia katika awamu ya mwisho ya ziara yake ya siku 12 katika mataifa ya Amerika ya Kusini.

Ziara yake ya siku tatu nchini humo itajumulisha mkutano wake na rais wa Colombia, Alvaro Uribe, wabunge na viongozi wa mahakama kuu.

Colombia inatarajiwa kuiomba Ujerumani iushawishi Umoja wa Ulaya kwa biashara huru na uungwaji mkono katika vita vyake dhidiy a biashara haramu ya dawa za kulevya.

Ujerumani kwa sasa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya na uenyekiti wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani, ya G8.