1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA: Rais Uribe aapishwa

8 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNn

Rais wa Colombia, Alvaro Uribe, ameapishwa kuiongoza nchi hiyo kwa awamu ya pili. Katika sherehe ya kuapishwa kwake, Uribe ameahidi kufanya mazungumzo ya kufikia mkataba wa amani na waasi wa mrengo wa shoto na kumaliza miongo minne ya vita vya wenyewe wa wenyewe nchini humo.

Wakati huo huo, rais Uribe amesema ataendeleza sera kali za usalama zilizopunguza visa vya mauaji na utekajinyara nchini Colombia.

Maelfu ya watu walikuwa wakiuwawa au kupoteza makaazi yao kila mwaka katika machafuko yaliyosababishwa na biashara ya madawa ya kulevya aina ya kokeini.