BOGOTA: Rais Köhler aendelea na ziara yake Amerika ya Kusini
13 Machi 2007Matangazo
Rais wa Ujerumani Horst Köhler yamo nchini Colombia katika awamu ya mwisho ya ziara yake ya siku 12 katika mataifa ya Amerika ya Kusini.
Ziara yake ya siku tatu nchini humo itajumulisha mkutano wake na rais wa Colombia, Alvaro Uribe, wabunge na viongozi wa mahakama kuu.
Colombia inatarajiwa kuiomba Ujerumani iushawishi Umoja wa Ulaya kwa biashara huru na uungwaji mkono katika vita vyake dhidiy a biashara haramu ya dawa za kulevya. Ujerumani kwa sasa inashikilia urais wa Umoja wa Ulaya na uenyekiti wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani, ya G8.